Habari

Mhe. Shonza atumia kauli ya Rais Magufuli kumuonya Gigy Money na wenzake, kuhusu picha za uchi mitandaoni

Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli kuwaonya wale wanaotumia mitandao ya kijamii kumong’onyoa maadili hapa nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Mh. Shonza ameitumia kauli hiyo iliyotolewa na Rais asubuhi wakati wa makabidhiano ya kifaa kitakachotumika katika mawasiliano ambacho TCRA wamekabidhiwa ambapo Rais alisema katika moja ya kauli wakati anaelezea madhara ya mitandao ya kijamii na kusema kuwa “Mitandao ya Kijamii inaleta sana mmong’onyoko wa maadili, TCRA washughulikieni wanaotumia mitandao hiyo kuharibu maadili”

Baada ya kauli hiyo Mhe.Shonza ambaye ni Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, yaani Naibu anayeshughulikia mambo yaote yanayohusu habari na mawasiliano ameipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema ” Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_ogna wenzio,msidhani hatuwaoni , “ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa”

Hii ndio ilikuwa hotuba yote ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli asubuhi TCRA :-

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents