Habari

Mhe. Tundu Lissu asema wanaohama Chadema hawawezi kuua chama hicho, amtaja Dkt. Slaa

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu amesema wanasiasa wanaohama chama hicho hawawezi kukifanya kufa.

Mhe. Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki katika mahojiano na kituo cha runinga cha Azam amesema viongozi mbalimbali kama Dkt. Wilbroad Slaa wameondoka lakini bado chama hicho kinaendelea.

“Mbunge wa kwanza kabisa wa Chadema katika historia ya vyama vingi vya nchi yetu anaitwa Amani Kabudi, ndio alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza na mimi nilipojiunga na Chadema miaka 13/4 iliyopita alikuwa Makamu Mwenyekiti na mbuge wa Kigoma mjini, aliishia wapi?,” Lissu amehoji.

“Baada ya kuhamia CCM Chadema ilikufa, Dkt. Slaa Katibu Mkuu na mbunge wa Chadema kwa vipindi vitatu mfululizo baada ya safari kuwa ndefu mno akashukia njiani, Chadema imekufa,” amesema Lissu.

Lissu amesema watu wanashangaa kuona wanasiasa wakihama chama hicho sababu mbali mbali aidha hawajui, wanasahau au kujisahaulisha lakini ni jambo ambalo lipo katika histori ya vyama vyingi hapa nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents