Habari

Mhitimu wa Chuo Kikuu anayetumia vituko vyake kuuza matango na embe “watu wananiona ni chizi” (Video)

Bongo5TV wiki hii imekutana na mhitimu wa Chuo Kikuu, Canaly Maswage ambaye kwa mara ya kwanza alionekana viwanja vya usaili wa mashindano ya kusaka vipaji Tanzania ya BSS ambao ulifanyika wiki iliyopita hapa Dar Es Salaam.

Kijana huyo alionekana maeneo hayo akiuza matango na embe pamoja na kujaribu bahati yake kupitia mashindano hayo huku akiimba nyimbo mbalimbali ambazo ziliibua gumzo mitandaoni.

Akizungumza na Bongo5, Kijana huyo alisema watu wengi wanamchukulia kama chizi lakini yeye kupitia biashara hiyo na vituko vyake anaingiza zaidi ya tsh 40000 kwa siku.

Canaly ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu, amesema aliamua kuingia kwenye biashara hiyo baada ya kuona hali ya ajira ni ngumu na kitu anachoweza kufanya na kumkomboa ni kujiajiri kupitia biashara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents