Michezo

Miaka 11 baadaye: Mtoto aliyenusurika kifo baada ya tsunami na kusaidiwa na Ronaldo asainishwa na Sporting Lisbon

Klabu ya soka ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno, imemsainisha kijana aliyenusurika kifo kwenye tetemeko wimbi la tsunami nchini Indonesia, Martunis kwenye academy yao, ikiwa ni miaka 11 baada ya janga hilo lililomfanya aokoe maisha yake kwa kukaa kwenye dimbwi la maji kwa siku 21 huku mama yake na kaka zake wawili wakipoteza maisha.

2A2AE0EE00000578-3147052-image-a-47_1435833952840
Martunis akiongea wakati wa kutangazwa kuchukuliwa na Sporting Lisbon

Martunis, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 17, alitangazwa kwenye mji mkuu wa Ureno, Lisbon baada ya kuwa na ndoto ya kucheza soka la kulipwa, licha ya uharibifu mkubwa uliofanywa na mafuriko hayo nchini Indonesia, December 26, 2004.
2A2B7E3900000578-3147052-image-a-1_1435849342017
Kijana huyo ameingizwa kwenye academy ya Sporting na msimu ujao anaweza kucheza kwenye timu ya wachezaji walio chini ya miaka 19

Mafuriko/mawimbi hayo makubwa yalisabibishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari ya Hindi na kuua watu 230,000 katika nchi 14.

2A2AFE5200000578-3147052-image-a-65_1435835254872
Wimbi la Tsunami ni miongoni mwa majanga ya asili mabaya zaidi kuwahi kutokea duniani

Sasa Martunis ameungana na chuo hicho maarufu cha Sporting kilichokikuza kipaji cha mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Luis Figo.

2A2A58F100000578-0-image-a-29_1435832963764
Martunis akiwa na Ronaldo

‘Ni jambo kubwa kuwa hapa, klabu hii inaifanya ndoto yangu iwezekane,” alisema kijana huyo. “Nimefurahi mno kwa fursa hii. Viva Sporting.”

2A2ADBF700000578-3147052-image-m-49_1435833999707
Martunis akiwa kwenye dimba la Estadio Jose Alvalade

Ronaldo alikutana na Martunis baada ya janga hilo baada ya picha zake akiwa na jezi ya Ureno aliyokuwa ameivaa wakati wa akicheza mpira muda ambao tetemeko hilo lilitokeo ziliposambaa mtandaoni.

2A2ABB0600000578-0-image-a-31_1435833309083
Martunis alipatikana akiwa na jezi ya Ureno kwenye fukwe za Banda Aceh, baada ya kukaa kwa siku 21

Martunis alikuja kuonana na baba yake lakini mama na kaka zake wawili walikuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwenye janga hilo kubwa la asili kuwahi kutokea duniani.

page
Martunis akiwa na Ronaldo na rais wa FIFA, Sepp Blatter

Nyumba ya mtoto huyo aliyekuwa na miaka saba ilijengwa kwa kutumia fedha zilizotumwa na chama cha soka cha Ureno na kukusanywa kwa jitihada za Ronaldo za kuchangisha fedha.

Ronaldo na mtoto huyo walikuja kukutana miaka mitatu baadaye.

Ronaldo aliyeanza kuchezea soka kwenye club hiyo aligharamikia elimu yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents