Michezo

Miamba ya Sportpesa uso kwa uso kwa mara ya kwanza Taifa

Klabu ya Yanga na Singida United  ambazo zote zina dhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri(Sportpesa) zinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki Agosti 12 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara

Mara baada ya mchezo huo Yanga ambayo ni mabingwa wa ligi kuu wanatarajia kucheza mchezo mwingine wa kirafiki na timu ambayo itatangazwa hapo baadae.

Katika hatua nyingine Kocha George Lwandamina ametoa mapumziko ya siku mbili za wikiendi kwa wachezaji wake na watarejea tena jumatatu asubuhi kuendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents