Michezo

Michael Carrick aanza kujiandaa na maisha ya kuwa kocha

Mchezaji wa klabu ya Manchester United Michael Carrick amekuwa na mipango ya kuwa kocha baada ya kustaafu kucheza soka.

cariki-2

Kiungo huyo Muingereza ambaye saivi ana miaka,35, hadi saivi ameitumikia Man United kwa miaka 10,mwezi juni mwaka huu alisaini mkataba mpya wa miezi 12 kunako timu hiyo na tayari ameshaanza kujiandaa na maisha yake baada ya kutundika daruga Carrick alionesha kuwa sasa yupo katika mafunzo ya ukocha baada ya ku post picha katika mtandao wake wa instagram.

cariki

Carrick ambaye amekuwa akitumia kipindi hiki cha mechi za kimataifa kuipata beji ya ukocha na sasa anapigania kupata leseni A ya UEFA.

Ina onekana Carrick na yeye anafuata nyayo za wachezaji wenzake wa zamani kama vile Nicky Butt,Ryan Giggs , Gary Neville na Phil Neville

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents