Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Michael Olunga ampagawisha kocha wake huko Sweden

By  | 

Baada ya dhiki ni faraja, Afrika Mashariki imeanza kung’ara kwenye soka la Ulaya baada ya kuteseka kwa muda mrefu.

url

Aliyekuwa mshambuliji wa timu ya Gor Mahia inayoshiriki ligi kuu ya nchini Kenya amezidi kufanya vizuri kwenye timu yake mpya ya, IF Djurgarden baada ya kuifungia timu yake hiyo bao lake la pili tangu ameanza kuichezea timu hiyo.

Kocha wa timu hiyo, Per Pelle Olsson amesema Olunga ni mchezaji mwenye uwezo wa kusoma mechi.

“Olunga ni mchezaji mzuri sana. Pia anaonyesha kwamba ana uwezo wa kusoma mechi. Ni mchezaji mwenye kasi licha ya ukubwa wake, kwa hivyo kwa jumla atatusaidia sana kwa upande wetu.” alisema Olsson.

IF Djurgarden ilicheza na Elfsborg, kwenye mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW