Michezo

Michael Schumacher apata ajali, hajitambui na hali yake ni mbaya

Mshindi wa mara saba wa mashindano ya Formula One, Michael Schumacher, anapigania uhai wake baada ya kupata madhara kwenye ubongo wake kufuatia ajali aliyoipata jana wakati akicheza michezo ya kwenye barafu.

3-67

Schumacher alikuwa hajitambui na hali yake ilikuwa mbaya baada ya kichwa chake kugongwa mwamba kwenye milima ya barafu ya Ufaransa ( French Alps). Mke wa Schumacher, Corinna na wanae wawili wamedaiwa kuwa naye hospitali alikolazwa.

Awali uongozi wa Schumacher ulidai kuwa alikuwa amevaa helmet wakati anapata ajali hiyo. Msemaji wa dereva huyo wa zamani wa mbio za magari, Sabine Kehm alisema kwenye maelezo yake: Michael fell on his head when he was on a private skiing trip in the French Alps.

Kutokana na ajali hiyo, dereva huyo wa Ujerumani mwenye miaka 44 alifanyiwa upasuaji wa ubongo.

“He remains in a critical condition,” alisema Kehm.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents