Technology

Microsoft kuununua mtandao wa kijamii wa LinkedIn kwa dola bilioni 26.2

Kampuni ya Microsoft imetangaza kuwa inaununua mtandao wa kijamii wa LinkedIn kwa dola bilioni 26.2.

image

Mtandao huo hadi sasa una watumiaji milioni 433 na hutumiwa zaidi kwa masuala ya kazi.

Manunuzi hayo ni ya fedha taslimu.

Kwa Microsoft, LinkedIn itaipa fursa kubwa katika biashara ya mitandao ya kijamii hasa yenye maudhui ya masuala ya kazi na biashara.

Mtandao huo hutumiwa zaidi na waajiri na waajiriwa na hivyo kampuni hiyo imepata sehemu ya kuuza zaidi bidhaa zake.

Mtandao wa LinkedIn upo katika zaidi ya nchi 200 duniani huku ikiwa na watumiaji hai zaidi ya milioni 105 kila mwezi na waliojiunga wakiwa milioni 433.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents