Habari

Kesi za ardhi zapungua Morogoro

Wakazi wa Kata ya Mngazi, Wilaya ya Morogoro wamesema migogoro ya ardhi iliyokuwa imekithiri katika maeneo yao imepungua kutokana na ushirikiano wao huku kesi hizo katika baraza la ardhi zikiwa zimepungua.

Wananchi hao wamesema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa katika kata hiyo kwa nia ya kufahamu namna migogoro ya ardhi inavyotatuliwa maeneo ya vijijini.

“Migogoro ya ardhi imepungua kutokana na wananchi kutambua njia sahihi ya kutatua migogoro na namna ya kuepuka isitokee tena katika maeneo yetu kwani watu wengi wameuawa na wengine kujeruhiwa,” alisema Asha Ally.

Amesema migogoro ya ardhi iliyokuwa inasumbua katika eneo lao ni pamoja na mipaka, mashamba ya urithi na baadhi ya viongozi wa vijiji kuuza maeneo bila ya kuwashirikisha wananchi, lakini hivi sasa haipo tena kutokana na wengi kupata uelewa, kujua nia sahihi ya kutatua na madhara ya migogoro ya ardhi.

Hata hivyo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Vigolegole, Octavian Kobelo amesema hivi sasa kesi za ardhi katika baraza la ardhi kata zimepungua na kuwa, kabla ya mradi huo walikuwa wanapokea kesi 10 kwa mwezi, lakini kwa sasa kesi moja inapokelewa na kufanyiwa kazi.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents