Burudani ya Michezo Live

Mikakati ya mwisho Mexicana Lacavera

Lacavela_Ajiba_face
(Ajiba mwanamuziki wa Mexicana)

Wasanii kutoka kundi la Mexicana Lacavera limeeleza mikakati yao mwisho kwa mwaka huu kwa kusema wanaachia wimbo wa mwisho mpaka mwakani ndipo watatoa mwingine.  Kiongozi wa kundi hilo Baghdad alisema kufanya hivyo ni kutoa nafasi kwa msanii mmoja mmoja.


wa kundi hilo ili aweze kutoa ngoma yake, ambayo itamtambulisha ili wasanii wote wa kundi wajulikani kwa kazi zao na uwezo wao. Amesema huwa kawaida yao kutoa nyimbo moja kila baada ya miezi sita, ili nyimbo zao ziweze kutamaniwa na wengi, kwani hivyo sasa wamejipanga kuachia ngoma ya  mwisho kwa mwaka huu, utakao kwenda kwa jina la Ona.

Lacavela_Baghdad
(Baghdad Kiongozi wa kundi la Mexicana)

Amese baada ya hapo kila msanii sasa atakuwa akianchia wimbo, lakini pia wapo tayari kwa mtu akitaka kuwashirikisha kama kundi au kumshirikisha msanii mmoja mmoja, katika wimbo wake. Wakali hao wa wimbo wa Full Ng’ae ng’ae  wamesema kwamba,  wimbo wa Ona wanautoa Special kwa mashabiki wao hadi mwakani.

Lacavela_fidodido
(Fidodido a.k.a Yekeyeke, Edo, mkali wa sauti, na ndiye aliyeweka sauti nzito kwenye Full Ng’ae Ng’ae)

Baghadad aliongezea kwa kusema mwakani wanaweza kurudi katika mtindo mwingine, huenda wakawa wanatoa nyimbo mpya kila baada ya mwenzi, wakatoa filamu au kujishughulisha na shughuli nyingine kama Mexicana Lacavera.

Lacavela_jokeri
(Joker toka Maxicana)

Pia Badhadad amesema katika wasanii wote wa Mexicana watakuwa wakitoa ngoma zao, lakini kasoro msanii mmoja Klimax, yeye ndiye ameachana na muziki kwa mwaka huu. Amesema kwamba mwanamuziki huyo atakubali kushirikishwa kwenye nyimbo ya mtu, na pia akiwa katika kundi lakini hatutoa wimbo wake akiwa yeye mwenyewe.

lacavela_Kush
(Mwanadada Kushi kutoka kundi la Mexicana, wenyewe ndiyo wanaamini msichana anayechana kuliko wote kwa sasa)

Klimax alisikika katika stesheni moja akihojiwa na kusema kukaa mbali na muziki kwa sasa ni kutokana na Watangazaji ‘Mapresenter’ wanaoogngoza vipindi vya muziki kumdai mkwanja kila anapopeleka kazi zake.

Lacavela_Tana_Diva
(Tana Diva mwanadada kutoka kundi hilohilo la Mexicana)

amekaririwa akisema kwamba kwakuwa muziki wa Bongo kama hauna mkwanja huwezi kutoka hata kama utakuwa na nyimbo mzuri, kwakuwa hujamshikisha kitu chochote mtu wa kupiga nyimbo zako. Amesema alichoamua ni kuacha na muziki kwa muda ili atafute fedha za kuwapa kama wanahitaji fedha.

Klimax alizidi kubonga na stesheni hiyo kwakusema kwamba, hivi sasa atajishughulisha zaidi na uuzaji wa nguo katika duka la kaka yake pande za Sinza. Presnter huyo, naye alitoa wasaha wake kwa Mapresenter wenzake waache tabia hiyo, kwani wanalipwa na waajiliwa wao . mimi pia kama Mo One na Bongo5 naungana na Presenter huyo kwa kulaani kitendo hicho, kwani wasanii wanapata fedha kidogo sana kutokana na kuibiwa kwa kazi zao, na wengi wao wanatokea katika maisha ya kipato cha chini.

lacavera

Mwisho wa siku likaja pozi kati ya Ajiba na Tana

Hebu sikiliza wimbo wa mwisho kwa mwaka huu wa Mexicana Lacavera…..ONA
{mmp3}mexicana-ona.mp3{/mmp3}

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW