Burudani

Mike Tee adaiwa kushiriki kumtapeli Bob Junior

Katika wimbi la utapeli linalozidi kuwakumba mastaa wa bongo,wakiwemo Ali K, Sajuki na sasa yamemkuta Bob Juniour ambapo safari hii, mdogo wake msanii wa Bongo Flava J.I,ambaye amewahi kutoka na wimbo wa ‘Kidato Kimoja’ amehusika moja kwa moja kumtapeli Bob Junior maeneo ya Rock City Mwanza, ambapa mdogo wake J.I alitoa namba ya simu ya Bob Junior kwa matapeli, na ndipo waliponayka dili ya kutoka kwa promota aliyemtaka Bob Junior kupiga show, na kutuma kabisa na pesa za advance ya kupiga show hiyo.

Promota huyo hakusita kuituma fedha taslmiu shilingi laki nane kwenye namba hiyo iliyokua imefanyiwa ujanja na ndipo matapeli baada ya kupokea fedha hizo kuzima simu hiyo na kutoweka.
Promota kuona kimya,alifanya jitihada kumpata Bob junior kusudi shughuli isiende mramba. Bob Junior alikana kuzungumza na mtu yeyote kuhusu show Mwanza na zaidi kukanusha kupokea pesa kutoka kwa mtu yeyote. Promota alikabidhi kazi polisi na kumnasa mdogo mtu J.I na alipofikishwa kituoni, alikiri kutoa namba ya Rais wa Masharobaro na kumtaja msanii na mfanyabiashara,Mike Tee, katika sakata hilo la kujifanya Bob Junior na hatimaye kutapeli fedha taslimu shilingi laki nane.

Bongo5 iliongea na Bob Juniour ambaye amewaonya wasanii wenzake kuhusu wimbi hilo lililoingia lakuswap simu za wasanii na wanajamii kwa ujumla na kuibiwa fedha. Ameomba mawakala kuwa makini zaidi na pia kampuni zinzoendesha mazoezi ya utumaji fedha pamoja na Serikali kuingilia kati kukomesha uwizi huu unaozidi kuongezeka.

Pia tulijaribu kumcheki Mike Tee,naye aligoma kuzungumzia issue hii na kuahidi kuizungumzia leo rasmi kwenye kituo cha radio ambapo baada tutakuletea updates.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents