DStv Inogilee!

Mike Tee ataja faida na hasara za msanii wa zamani kufanya collabo na msanii mpya ili arudi kwenye chati

Rapper mkongwe Mike Mwakatundu a.k.a Mike Tee, ameeleza mtazamo wake juu ya faida na hasara za msanii wa zamani (kama yeye) kumshirikisha msanii mpya anayefanya vizuri kwa sasa kwa lengo la kurudi upya kwenye chati baada ya kupotea.

mike tee

Mike amesema faida kubwa ya msanii wa zamani kumshirikisha msanii mpya ni kujipatia mashabiki wapya kutoka kwa msanii mpya hivyo kutanua wigo wa mashabiki wake pia.

Upande wa hasara Mnyalu amesema msanii husika anaweza kuonekana kabebwa na msanii mpya hivyo kuwa vigumu uwezo wake kupimika kirahisi. Alisema hayo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Hata hivyo mike amesema swala hili linategemea na mtazamo binafsi wa mtu.

Hivi karibuni rapper mwingine mkongwe, Jay Moe alisikika akisema aliamua kutomshrikisha msanii mkubwa kwenye ngoma ya ‘Hili Game’ ili kuonyesha uwezo wake kuwa hajabebwa na mtu.

Wakati huo huo Mike Tee ameachia wimbo mpya wiki hii, uitwao ‘Kiduchu’ ambao hajamshirikisha msanii yeyote, usikilize hapo chini.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW