Michezo

Mike Tyson chini ya ulinzi mkali Chile

Bingwa wa zamani wa dunia wa uzito wa juu Mmarekani, Mike Tyson amezuiliwa kuingia nchini Chile kufuatia kuwa na rekodi ya makosa ya kijinai.

Bingwa wa zamani wa dunia wa uzito wa juu Mmarekani, Mike Tyson

Vyombo vya habari vya Chile viliripoti kuwa Tyson alikuwa na mpango wa kuhudhuria sherehe za tuzo huko Santiago.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 51, anatuhumiwa kuhusika na ubakaji,kushambulia na madawa ya kulevya hali iliyopelekea kuzuiliwa  Uwanja wa ndege na askari wa uhamiaji.

Polisi wa uwanja wa ndege wa Santiago wamesema Tyson alizuiliwa kufuatia kukiuka sheria za uhamiaji.

Mwaka 2013, Mike Tyson alizuiliwa kuingia nchini Uingereza kufuatia kukutwa na hatia hizo.

“Kufuatia rekodi yake ya nyuma, sheria ya sasa ya uhamiaji inazuia wageni wowote wenye makosa ya kijinai kuingia ndani ya nchi.” Amesema polisi huyo.

Mike Tyson amekuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu akiwa na umri mdogo wa miaka 20 baada ya kumpiga Trevor Berbick mwaka 1986.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents