Burudani

MIKE WILL Made It azungumzia ujio wa albamu ya Rae Sremmurd.

Rae Sremmurd wamekuwa wakiifanya kazi albamu yao mpya iitwayo “SremmLife 3” kwa muda sasa. Na kwa mujibu wa Mike WILL Made It amesema tutarajie miziki mingi kutoka kwao.

Mike WILL Made It ambaye alishinda “Best Rap Song” katika tuzo za Grammy kwa ajili ya kuzalisha ngoma ya msanii Kendrick Lamar ‘HUMBLE’ aliliambia Pitchfork kwenye red carpet kwamba albamu hiyo itakuwa na sura tatu na ya kwanza ni ya Swae Lee iitwayo Swaecation na ya pili ni ya Slim Jxmmi iitwayo Jxmtroduction na kisha upande wa Rae Sremmurd.”

Mike WILL Made It alisema kuwa jina la albamu mpya ya Rae Sremmurd bado hawajaaamua lakini ni wanategemea kuwa albamuhiyo itaitwa “Sremmin.”

Wiki iliyopita waligusia katika kufanya ngoma na Kendrick Lamar kwa kutuma picha kwewnye mitandao wakiwa na rapa huyo studio. Albamu yao ya mwisho ilikuwa inaitwa SremmLife 2 walioachia Agosti 2016 ambayo ilikuwa na ngoma iliyo hit sana iitwayo ‘Black Beatles’ waliomshirikisha Gucci Mane.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents