Michezo

Mikoa mitatu yashiriki kutoa kozi ya ukocha

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ limeendelea na utoaji wa kozi ya makocha ili kupata waalimu wa kutosha katika kuliendeleza soka hapa nchini.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeongeza juhudi za kufundisha makocha wa mpira wa miguu hapa nchini ili idadi ya walimu wa mpira wa miguu wanaopaswa kushiriki kwenye programu za maendeleo ya vijana za mikoa.

Hii ni katika kukidhi malengo ya TFF katika kusimamia maendeleo ya soka la vijana hapa nchini.

Kwa sasa, TFF kwa kushirikiana na mikoa ya Songwe, Lindi na Kigoma, zinaendeshwa kozi ngazi ya awali (Preliminary) na ngazi ya kati (Intermidiate).

Katika mkoa wa Songwe kozi ya ukocha zinazoendeshwa ni kozi ya awali Wilaya ya Songwe inayoendeshwa na Mkufunzi John Simkoko na kozi ya awali, wilaya ya Tunduma inaendeshwa na Mkufunzi George Mkisi.

Mkoani Lindi kozi ya awali ilianza Septemba 11, 2017 katika Wilaya ya Kilwa ikiendeshwa na Mkufunzi Michael Bundala na mkoani Kigoma kuna kozi mbili zinaendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents