Burudani

Mikosi juu ya mikosi: Baada ya Celin Dion na Lady Gaga kutangaza kuzifuta kolabo zao na R.Kelly leo Chance the Rapper nae kaibuka na hili

Mashtaka yanayoendelea kumuandama nguli wa R&B duniani R.Kelly, yanaendelea kumzoofisha kwani kila siku yanatokea mapya kuhusiana na staa huyo.

Likiwa saka hilo linaendelea huku wakijotokeza wadau mbalimbali pamoja na wasanii wakitoa maoni yao na misimamo yao juu ya hilo bado kuna mapya yanaendelea kujitokeza.

Siku ya jana mwimbaji Celine Dion aliapa kuifuta colabo yake na R. Kelly ya “I’m Your Angel” kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kupakua nyimbo mitandaoni kufuatia tuhuma zake za unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo.

licha ya wimbo huo kuwa na takribani miaka 21 hadi hivi sasa tangu utoke na, tayari umeuza nakala milioni 2 kwa Marekani.

Msanii mwingine aliyetoa kauli ya kufuta kolabo yake na R.Kelly ni Lady Gaga, baada ya kutangza kuifuta ngoma ya “Do what you want” ya mwaka 2013, leo tena amejitokeza mshikaji ambaye hapo nyuma alikataa kauli hii, huyu sio mwingine bali ni Chance the Rapper.

Chance The Rapper ameifuta colabo yake na R.Kelly “Somewhere in Paradise” ya mwaka 2015 kwenye mitandao ya kusikiliza na kupakua nyimbo mtandaoni kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo ambazo zinaendelea kumtafuna nguli huyo. Hivi karibuni Chance alitoa taarifa kuwa anajutia kuwahi kufanya kazi na Kelly, alisema ilikuwa ni kosa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents