Bongo Movie

Milion 25 yakatika kwenye Mr President

Stive_Nyerere_face

Mwigizaji wa filamu Tanzania, Stive Nyerere ambaye filamu yake ya Mr Predent imeingia mtaani juzi baada ya kuzinduliwa na mbunge wa viti maalum wa Ccm,  Vick Kamata na hatmaye kuuzwa kwa mnada Cd hiyo, amesema kwamba kwamba haogopi hasara kutokana na gharama kubwa aliyotumia.

Filamu hiyo ya Mr Presedent, imekatika shilingi milioni 25, mpaka inaingia sokoni jambo ambalo anamatumaini ya kurudi na kwamba hata kama haikurudi itakuwa ni heshima kwake na sio lingine.

Amesema gharama yote hiyo ilitokana na ushirikiano mdogo aliokuwa akikutana nao katika kuiandaa filamu hiyo, kuanzia kwenye majumba kama Ikulu na ofisi zingine za Serikali, pamoja na kuwakusanya watu kwaajili ya vikao.

Stive_Nyerere

Stive Nyerere anasema filamu hiyo tayari imeshaanza kuombwa na watu wengi, huku akipokea simu kutoka mikoa mbalimbali wakimtaka aifikishe huko mapema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents