Burudani

Millard Ayo aeleza sababu ya usiri kwenye mahusiano yake na mpango kufungua Redio na TV

Mtangazaji mwenye ushawishi zaidi Tanzania kwa mujibu wa The Africa Youth Award, Millard Ayo amefunguka kuzungumzia kuhusu maisha yake pamoja na mpango wa kufungua kituo chake cha Redio na TV.

Millard Ayo

Millard ambaye anaendesha kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM pamoja na mtandao wa habari Millardayo.com, amesema yupo kwenye mahusiano lakini anashindwa kumuanika mpenzi wake kwa kuwa hataki mambo ya mtandaoni.

“Ninaye, simpost kwa sababu yeye mwenyewe hataki, sio mtu wa media kabisa, hapost sura yake popote,” Millardayo alikiambia kipindi cha 360 cha Clouds TV mapema asubuhi ya leo.

Katika hatua nyingine mjasiriamali huyo kijana, amedai kwa sasa hana mpango wa kufungua runinga yake pamoja na redio kwa madai bado anaona fadhila ambazo alipewa na Clouds Media hajazirudisha.

“Watu wananiambia nifungue Redio na Tv yangu, lakini mimi naona bado. Bado kwa sababu naona Clouds inanidai, mimi siidai. Clouds imenifanyia mengi, sioni kama naweza kuwalipa kwa hiyo nikifanya kazi hapa najisikia vizuri. ”  alisema Millardayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents