Picha

Millen Magese achangia ujenzi na vifaa vya shule mkoani Mtwara

Well guys, Tanzania international fashion and beauty export, Millen Magese alikuwa Tanzania couple days ago for a charity mission, kukabidhi vitu mbali mbali kama msaada kwa wana Mtwara. Millen ambae kwa sasa anaishi nchini Marekani akijishughulisha na fani ya mitindo akiwa Mtwara alipokelewa na viongozi mbalimbali wakiwamo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara; Mhe. Willman Ndile, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, imbakali na Mbunge wa Mtwara mjini; Mhe. Hasnain Murji.

Millen Magese akipokelewa na Mheshimiwa Ndile pamoja na Afisa Elimu manispaa ya Mtwara, Mama Florah Aloys
Millen Magese akipokelewa na Mheshimiwa Ndile pamoja na Afisa Elimu manispaa ya Mtwara, Mama Florah Aloys

Millen donated a total of 15 millions Tanzania Shillings, whereby 10 millions Tanzania Shillings will be for the re construction of Mjimwema primary school block which Magesse was touched by its deteriorated condition when she toured the school earlier on the day during her official Mtwara tour. The remaining 5 Million was donated to Lililungu primary school which was used for school desks for students to sit on them.

Millen Magese akikabidhi hundi ya milioni kumi na tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mhe. Wilman Ndile; kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hasnain Murji
Millen Magese akikabidhi hundi ya milioni kumi na tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mhe. Wilman Ndile; kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hasnain Murji

Shule hiyo yenye madarasa mawili yaliyojengwa kwa udongo ambapo wanafunzi wakiwa ni wengi huku wengi wao wakiwa hawana viatu na sare zao za shule zikiwa zimechakaa.

Millen Magese akipokelewa na mkuu wa Mkoa Mtwara , Mhe. Simbakalia, pembeni yake ni Mbunge wa Mtwara, Mhe. Hasnain Murji
Millen Magese akipokelewa na mkuu wa Mkoa Mtwara , Mhe. Simbakalia, pembeni yake ni Mbunge wa Mtwara, Mhe. Hasnain Murji

Akizungumza shuleni hapo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndile, Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamitindo ameguswa na hali mbaya ya mazingira ya shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wanasomea katika shule ya udongo huku wakiwa na mazingira duni ya kufundishia.

Millen magese akiongea na wanafunzi na walimu wakati wa ziara yake mashuleni
Millen magese akiongea na wanafunzi na walimu wakati wa ziara yake mashuleni

Aliongeza na kusema, “Mwaka 2001/2002 nilitembelea mkoa wa Mtwara ambao ulinigusa sana kwenye swala zima la elimu, haswa mazingira ambayo yanamfanya mtoto akae chini. Na nikaahidi siku moja Mungu akijalia nitarudi Mtwara na nimesikitika ni miaka 12 sasa bado watoto wanakaa chini nikaone nirudi kutimiza ahadi na kutoa hamasa kwenye swala hili la elimu mkoani Mtwara.” Mbali na milioni kumi na tano pia aliahidi kuwatafutia sare za shule wanafunzi hao jozi mbili kila mmoja na pia alikubali kuwa mlezi wa shule hiyo.

 Millen Magese akisalimiana na mwenyekiti wa UWT, Mama Sophia Simba, kulia kwake ni Mhe. Simbakalia
Millen Magese akisalimiana na mwenyekiti wa UWT, Mama Sophia Simba, kulia kwake ni Mhe. Simbakalia

Pia alipata fursa ya kukaa na wajasiriamali walioandaliwa semina na mkuu wa wilaya pamoja na mbunge wa Mtwara mjini kujadili mbinu za kuwaongezea kipato na kwa kuanzania milioni sita iliyopatikana iligawanywa kwa wajasiriamali kulingana na vikundi ili wao watengeneze madawati kwa ajili ya watoto wao, ambapo milioni tano ilitolewa na Millen Foundation na milioni moja ilitolewa na Mhe. Murji

 Millen Magese akipiga picha na mashabiki wake waliokuja kumpokea uwanja wa ndege mjini Mtwara
Millen Magese akipiga picha na mashabiki wake waliokuja kumpokea uwanja wa ndege mjini Mtwara
 Millen Magese akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mashuleni.
Millen Magese akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mashuleni.
Naye mkurugenzi wa manispaa alisema Millen ameweka historia kwani kitu hiki hakijawahi kufanyika Mtwara na mtu binafsi wanaangalia ni jinsi gani Millen Magese atakumbukwa kama muanzilishi wa ujenzi wa shule ya mji mwema.

28

Baada ya kuzungumzia ahadi yake hiyo Millen aliwahamasisha wadau wengine aliiongozana nao kuchangia mchango wa shule hiyo akiwamo Mbunge wa Mtwara mjini Murji ambae aliahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi zaidi wa shule hiyo na shilingi milioni moja kwa ajili ya madawati.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara; Mhe Ndile pamoja na Mhe. Murji waliwataka wananchi kuhamasika zaidi kwa kuunga mkono harakati za Millen katika kuimarisha elimu mkoani humo kwa kuwa ameonesha mfano mzuri akiwa kama mwanamitindo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents