Mitindo

Millen Magese Awataka Wanamitindo Kuchangamkia Nafasi


Mwanamitindo wa Kimataifa wa Tanzania, Millen Magese anayefanya shughuli zake za mitindo nchini Marekani ataendesha zoezi la kutafuta wanamitindo wawili (mmoja wa kike na mmoja wa kiume) watakaoshiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya wiki ya mavazi Afrika kusini(South Africa Fashion week) tarehe 1 April mwaka huu.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari mwanamitindo huyo ambaye ni Miss Tanzania wa mwaka 2001 alisema atafanya zoezi hilo kupitia kampuni yake ijulikanayo kama Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo Tanzania International Fashion Expose (TIFEX). Magese aliendelea na kusema wanamitindo wanaotaka kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika South Africa Fashion Week watatakiwa kufika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar-Es-Salaam, siku ya jumapili tarehe 25, kuanzia saa 8 mchana.

Aidha Magese aliongelea madhumuni ya yeye kutoa nafasi hiyo ambayo haina gharama yeyote kwa yule atakayekuwa anawania kupata nafasi hiyo ni pamoja na kuipatia nchi ya Tanzania nafasi ya kujitangaza kimataifa kupitia kazi hizo za urembo na pia kuwa ajira kwa watakaopita.

Aliongeza kwa kusema lengo kubwa la kwake na kampuni yake ni kuendeleza fani ya mitindo, ubunifu na urembo na vilevile kuitangaza Tanzania kwa kuongeza namba ya wanamitindo wa kimataifa watakaokuwa wanafanya kazi kwenye miji mikubwa kama London, New York, Milan, Paris etc zaidi ya yeye na Flaviana Matata ili kuwa sawa na wanamitindo wa nchi kama Afrika Kusini na Nigeria ambao wako wengi.

Alivitaja vigezo vitakavyotumika kwa wale watakaokuwa wanawania nafasi hiyo ni pamoja na umri wa miaka 18 mpaka 24, urefu wa 1.75 m, hips 37 cm pamoja na kuwa na nywele za asili. Kwa wanaume urefu ni 1.82m.

Bongo5 inakupongeza sana kwa juhudi za kusaidia kuibua vipaji vitakavyoinua tasnia ya urembo na jina la nchi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents