Tupo Nawe

Mimi si mali ya mtu na wala sipo kwa ajili ya kujiuza – Wastara

Msanii wa filamu nchini ambaye siku za karibuni aliomba talaka kutoka kwa mume wake amefunguka na kusema yeye sio mtu wa kujiuza, bali ni mtu ambaye anajijali na kujitunza.
Wastara Juma

Muigizaji huyo ambaye alikuwa ni mke wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma, aliomba taraka baada ya mambo kumshinda.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Wastara ameweka wazi nia yake ya kutafuta mwaume mwingine.

“Mimi si mali ya mtu na wala sipo kwa ajili ya kujiuza, lakini ukweli ni kwamba wapo wanaume wa aina nyingi ambao wanakuja na kunitaka wengine wanakuja wakitaka ndoa kabisa na wengine unakuta kweli wanania ya dhati kabisa lakini wanakuja wakati mimi sijisikii kuwa na mwanaume, maana kitu kwa kitendo alichonifanya Sadif hakijaniweka sehemu nzuri,” alisema Wastara.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW