Burudani

Mimi siamini kwenye kulogwa – Stamina

Msanii wa hip hop Bongo, Stamina amedai haamini kuwa mtu anaweza kulogwa katika muziki.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘International Local’ ameiambia Magic Fm kuwa kupanda na kushuka kwa msanii ni sehemu ya maisha.

“Kulogwa sijawahi kuhisi, siaminigi kwenye kurongwa kwa kuwa namuamini sana Mwenyenzi Mungu, nahisi unakuwa muda wako bado, unajua kuna muda wako bado na muda wako si sahihi. Muda ukiwa bado ina maana kuna vitu huwezi kuvipata lakini muda si sahihi ina maana kuna vitu ulivipata lakini vimeshuka kidogo, hivyo inabidi ukaze ujue umekosea wapi urudi kwenye muda wako,” amesema Stamina.

“Ujue kudondoka ni moja kati ya step za maisha, cha msingi ni kuinuka na kuendelea na safari, kwa mfano sisi uwekezaji wetu mkubwa ni kwenye nyimbo unaweza ukatoa wimbo usifanye vizuri haimaanishi wewe ndio game yako imeisha, jua umekosea unarudi unaamsha tena dude  vitu vinaendelea,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents