Miriam Makeba Afariki Dunia

Mwanamuziki nguli kutoka Afrika ya Kusini ‘Miriam Makeba (76)’ amefariki mapema Jumapili huko mjini Italia alikokuwa kwa ajili ya onyesho, msemaji wa mwana mama huyo amedai mwanamuziki huyo amefariki katika kliniki ya Pineta Grande

Miriam Makeba Afariki Dunia

 

Mwanamuziki nguli kutoka Afrika ya Kusini ‘Miriam Makeba (76)’ amefariki mapema Jumapili huko mjini Italia alikokuwa kwa ajili ya onyesho, msemaji wa mwana mama huyo amedai mwanamuziki huyo amefariki katika kliniki ya Pineta Grande iliyopo Castel Volturno.

Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Italia vimedai mwanamuziki alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika kliniki hiyo.

Miriam Makeba, alipatwa na mshtuko wa moyo mara tu baada ya kufanya onyesho ambapo aliimba kwa takribani dakika thelathini kuonyesha mshikamano miongoni mwa waandishi wa habari wa kiitalia, baada ya  mwandishi mwenzao Roberto Saviano kupokea vitisho baada ya kuandika kitabu kuhusiana na Camorra, Naples eneo lijulikanalo kama kitovu cha uhalifu.

Habari ya kufariki kwa Makeba imeshtua raia wengi wa Afrika, Makeba alianza kutambulika kimataifa mara baada ya kutoka na dokomentari yake iliyojulikana kama ‘Come Back Afrika’ mnamo mwaka 1959, na Mwaka 1960 alipozuiwa alipokuwa akirudi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mama yake baada ya hati yake ya kusafiria kuwa na hitilafu.

Mwaka 1966 Makeba alipokea tuzo za Grammy kupitia kibao ‘An Evening with Belafonte/Makeba’ alichoshirikiana na Harry Belafonte.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema peponi. AMINA.

 

Bofya hapa chini kusikiliza uwimbo wa Malaika:

{mmp3}miriam_makeba_malaika.mp3{/mmp3}

 



 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents