Habari

Misri, Sudan na Ethiopia mambo sio shwari, nani mwenye haki na maji ya Mto Nile ?

Maafisa wa Misri na Sudan wamesema duru ya majadiliano kati ya mataifa matatu yaliyoko katika bonde la Mto Nile kuhusiana na mvutano wa bwawa la umeme nchini Ethiopia yalimalizika jana bila kupata makubaliano.

Egypt: Ethiopia's 'strict' stance on Renaissance Dam diminishes ...

Hali hiyo imeporomosha matumaini madogo yaliyokuwapo kwamba mataifa hayo matatu yanaweza kutatua tofauti zao na kutia saini makubaliano kabla ya Ethiopia kuanza kulijaza bwawa hilo.

Ethiopia hapo kabla ilitaka kuanza kulijaza bwawa hilo, bila ya kupatikana makubaliano kuhusu utaratibu wa kuliendesha, mwanzoni mwa msimu wa mvua katika mwezi Julai, wakati mvua zinaufanya tawi la mto Nile la Blue Nile kufurika.

Hata hivyo, fursa iliyotangazwa ya wiki mbili hadi tatu ya kutatua mzozo huo inakaribia kufikia mwisho kwa kasi. Kwa Ethiopia bwawa hilo linatoa fursa adimu ya kuwatoa mamilioni ya raia wake kutoka katika umasikini na kuwa nchi inayouza nishati ya umeme kwa wingi nje.

Nchi hizo mbili zimekuwa katika majadiliano ya ubishani kwa miaka kadhaa na bado hazijafikia makubaliano ya kugawana maji ya mto Nile.  Misri ambayo inategemea mto Nile kwa kiasi kikubwa kwa kilimo, viwanda na maji ya kunywa, imekuwa ikitafuta hakikisho kwamba bwawa hilo halitakata mtiririko wa maji kwa wakazi wake wanaozidi kuongezeka.

Ethiopia, ambayo nidiyo chanzo cha mto wa Blue Nile unaoungana na White Nile mjini Khartoum na kutiririka nchini Msiri, imesema kwamba bwawa hilo halitaathiri usambazaji huo na inatumaini kwamba mradi huo utaibadilisha nchi hiyo kuwa kitovu cha nguvu katika ukanda ulio na uhaba wa umeme.

Turudi nyuma kidogo hadi mwaka 1929

Makubaliano ya mwaka 1929 yalisainiwa kati ya Misri na Uingereza, ambayo kwa wakati huo iliziwakilisha nchi za Uganda, Kenya, Tanganyika hivi sasa Tanzania na Sudan. Mkataba huo uliipatia Cairo haki ya turufu ya kupinga miradi mikubwa inayoathiri sehemu yake ya maji.

Makubaliano ya 1959 baina ya Misri na Sudan. Makubaliano haya baina ya Misri na Sudan, kuongezea makubaliano ya awali, yaliipatia Misri haki ya ujazo wa bilioni 55.5 mita za maji ya Nile kwa mwaka na Sudan mita za ujazo bilioni 18.5 kwa mwaka. Makubaliano yote ya mwaka 1929 na 1959 yametengeneza chuki miongoni mwa mataifa mengine yanayotumia mto Nile na kutoa wito wa mabadiliko katika mkataba huo, yanayopingwa na Misri.

Mpango wa matumizi ya bonde la mto Nile

Mpango huu ulianzishwa mwaka 1999, uliyaleta mataifa tisa ya bonde la Nile ili kuuendeleza mto huo katika mazingira ya ushirikiano, kushirikiana faida za kiuchumi na kukuza amani ya kikanda na usalama. Mpango wa nchi tisa za bonde la Nile zilikuwa ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Misri, Ethiopia, Kenya, Sudan, Rwanda, Tanzania na Uganda. Tangu wakati huo Sudan Kusini nayo imeongezwa katika mpango huo.

Makubaliano ya Entebbe

BdT WM Qualifikation Ägypten Algerien Fußball (AP)Familia nyingi za Misri zinategemea shughuli za uvuvi katika mto Nile

Misri iliondoa uanachama wake katika mpango wa bonde la mto Nile mwaka 2010 baada ya nchi nyingine kusaini mkataba wa makubaliano wa CFA. Misri inadai makubaliano hayo yaligawa upya matumizi ya maji ya mto huo bila ya ridhaa yake.

Mkataba wa CFA unaojulikana kama makubaliano ya Entebbe, ulisainiwa na nchi sita kati ya 10 za mpango wa bonde la mto Nile. Nchi hizo ni Uganda, Ethiopia, Rwanda, Tanzania, Kenya na Burundi.

Misri inataka mbadala wa mkataba huo, ambao sasa unaruhusu nchi nyingine kuanzisha miradi katika mto huo bila ya ridhaa yake.

Mkataba wa ushirikiano wa 2015

Viongozi kutoka Misri, Ethiopia na Sudan walitia saini mkataba wa ushirikiano mwaka 2015 juu ya ujenzi wa bwawa kubwa katika jitihada kupunguza mvutano. Mkataba huo ulilenga kusafisha njia kwa ajili ya ushirikiano wa baadae wa kidiplomasia. Kanuni kuu katika makubaliano hayo ni pamoja na kutoa kipaumbele kwa nchi kutumia umeme utakaozalishwa katika bwawa hilo, njia inayoonekana kutatua migogoro na kutoa fidia kwa uharibifu.

SOURCE DW SWAHILI

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents