Michezo

Misri wang’ara AFCON, mashabiki 75,000 wajitokeza ufunguzi (Video)

Wenyeji wa michuano ya Kombe la Taifa Bigwa Afrika, Misri waeanza kampeini yao ya kuwania taji hili maarufu la soka Afrika kwa kuilaza Zimbabwe bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa mjini Cairo.

https://youtu.be/22hdfWIEED8

Mahmoud Trezeguet alifunga bao la kipekee la mchezo huo kabla ya muda wa mapumziko.

Mashambuliaji wa Liverpool Mo Salah alikaribia kutia kimyani bao la pili katika kipindi cha pili lakini kipa wa Zimbabwe Edmore Sibanda hakumpatia nafasi.

Ovidy Karuru aliipotezea Zimbabwe nafasi nzuri ya kusawazisha bao hilo la Misri katika mashambulizi ya dakika za mwisho.

Mashindano ya mwaka huu ya Afcon ambayo inajumuisha timu 24 ndio makubwa zaidi kuchezwa msimu wa joto wa Ulaya.

Sherehe ya ufunguzi wa mashindano hayo zilisheheni mbewe mbwe za kila aina huku mashabiki 75,000 waliojitokeza kushangilia timu yao ya nyumbani katika uwanja wa Kimataifa Cairo.

Lakini mchezo wenyewe haukufikia kiwango cha msisimko wa sherehe ya kuvutia ya ufunguzi baada ya Misri kutawala mchezo huo bila kumfikia kipa Sibanda wa Zimbabwe kama ilivyotarajiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents