DStv Inogilee!

Misri yapata kigugumizi kuthibitisha, Salah kuanza dhidi ya Uruguay baada ya hili

Chama cha soka nchini Misri kimeshindwa kuthibitisha kuwa mshambuliaji wake hatari, Mohamed Salah atakuwemo kwenye kikosi cha wachezaji watakao ikabili timu ya taifa ya Uruguay baada ya kumfanyia vipimo licha yakuwa na matumaini madogo ya uwepo wake uwanjani siku hiyo ya Ijumaa.

Mkurugenzi wa Chama cha Soka cha Misri Ehba Lehita amesema kuwa ”Anaendelea kuimarika ingawa nashindwa kuthibitisha kuwa Salah atakuwepo kwenye mechi yetu ya kwanza ya ufunguzi,” amesema Ehab Lehita.

Lehita ameongeza ”Yote ninaweza kusema tunamatumaini atakuwepo kwenye mchezo huu.

Nyota huyo wa klabu ya Liverpool amekuwa kwenye wasiwasi wa kushiriki michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kupata majeraha ya bega la kushoto wakati alipo ikabili Real Madrid hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Ulaya ambao timu yake ilipoteza kwa jumla ya mabao 3 – 1.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW