Habari

Miss Arusha afukuzwa nchini

Miss Arusha 2007Hatimaye imebainika kuwa Miss Arusha 2007 aliyejinyakulia zawadi ya gari ndogo aina ya Toyota Sprinter, Faith Msuya (22), ni raia wa Kenya na Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha, imemuamuru kuondoka.

Miss Arusha 2007


Hatimaye imebainika kuwa Miss Arusha 2007, Faith Msuya (22), siyo raia wa Tanzania na hivyo ameamriwa kuondoka nchini.


Mrembo huyo aliyejinyakulia zawadi ya gari ndogo aina ya Toyota Sprinter lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni tano, imebainika kuwa ni raia wa Kenya na Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha, imemuamuru kuondoka.


Ofisa Mkuu wa Uhamiaji mkoani Arusha, Justin Kabigumira, alikaririwa na gazeti hili Juni 15, mwaka huu, akieleza utata wa uraia wa mrembo huyo na kuwa Uhamiaji Makao Makuu wanalishughulikia suala lake, lakini uchunguzi wa awali umebaini kuwa siyo Mtanzania.


“Hatua ya awali ya mahojiano imeonyesha wazi kuwa mrembo huyo siyo raia wa Tanzania, bali ni raia wa Kenya, kwa kueleza kuwa wazazi wake wote ni Wakeny a kufuatia yeye mwenyewe kukiri, lakini bado tunamshikilia kwa mahojiano zaidi ya ndani,” Kabigumira aliwahi kukaririwa na gazeti hili.


Hata hivyo, uchunguzi zaidi wa gazeti hili katika Idara ya Uhamiaji Arusha, umebaini kuwa mrembo huyo aliamriwa na ofisi hiyo kuondoka nchini Julai 15, mwaka huu, baada ya kugundua kuwa siyo raia.


“Mrembo Faith alipewa amri ya kuondoka nchini Julai 15, mwaka huu baada ya uchunguzikukamilika na kubaini kuwa siyo raia na iliamriwa kurudisha zawadi zote, ikiwamo gari kwa kampuni ya Triple A iliyokuwa imeandaa shindano la kumtafuta mrembo wa Arusha,” alisema mtoa habari wetu.


Meneja wa Triple A, Herman Lushaka alipoulizwa kuhusu kurudishwa zawadi, alikiri urudishwa gari hilo na zawadi nyingine kutoka kwa mrembo huyo.


Herman alisema wao kama waandaaji wa mashindano hayo mwaka huu waliarifiwa na maofisa wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha kwenda kuchukua zawadi hizo.


”Tuliambiwa tukachukue za wadi ya gari tuliyompa mrembo kwani siyo raia na sisi tulitekeleza hilo bila kuchelewa,” alisema meneja huyo wa Triple A.


Hata hivyo, licha ya kufukuzwa nchini, mrembo huyo bado yupo na anafanya kazi Zamu International Dental Clinic iliyopo eneo la Mrefu nje ya mji wa Arusha.


Alipoulizwa kuhusu kushindwa kuondoka kwa mrembo huyo, Kabigumira hakuwa tayari
kulizungumzia suala hilo.


Mwandishi wa habari hizi alikutana ana kwa ana na mrembo Faith katika hospitali hiyo na hakuwa tayari kuzungumza sababu za kubaki nchini licha ya kuamriwa kuondoka.


”Sina cha kukujibu kwa sasa na sina nafasi ya kuongelea mambo hayo,” alijibu kwa kifupi mrembo huyo.


Mrembo huyo alikamatwa Juni 13, mwaka huu alipokwenda Uhamiaji kuomba fomu za maombi ya uraia wa Tanzania, ndipo kasheshe lilipoibuka na kuwekwa chini ya ulinzi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents