Habari

MISS DAR INTER COLLEGE KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA J’MOSI


WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar
Intercollege 2012 jumamosi hii wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa
kwa ajili ya kujifunza. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi
huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha
(IFM) Juni, 22 mwaka huu. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa
shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao
katika harakati zao za kielimu. Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu
kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria
vilivyopata kutokea katika karne zilizopita. ³Kama mjuavyo kule kuna kuna
fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine
vya kwanza kuanza kutumika,²alisema. Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa
ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya
IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na
Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo
Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi
Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi,
Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica
Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose
Masanja na Jamila Hassan. Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd¹s Original, Dodoma Wine, Ndege
Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters,
Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog
za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents