Miss Lushoto 2009

Miss Lushoto Irene Mahani (kati) akiwa amepozi na mshindi wa pili Jasmin Zaharan (shoto) pamoja na mshindi wa tatu Ashura Shabaan
Irene Mahani ametwaa taji la urembo la Wilaya Lushoto, baada ya
kuwazidi wenzake wanane katika mchuano mkali kwenye Ukumbi wa CCCM
Lushoto

Kwa ushindi huo Irene
amejinyakulia seti ya televisheni aina Sony yenye thamani ya TSh250,000, shindano hilo pia lilimshuhudia Jasmin Zaharani akiitwaa
nafasi ya pili na kujishindia seti ya muziki yenye thamani ya TSh200,000
wakati nafasi ya tatu ilitwaliwa na Ashura Shabaan aliondoka na
‘dressing table’ yenye thamani ya TSh150,000.
 
Nafasi ya
nne ilikwenda kwa Ashley Malika ambaye alijishindia deki na kusoma kozi
ya kompyuta, huku Fatuma Yusuf akishika nafasi ya tano na kujinyakuliwa
deki.
 
Mashindano hayo yaliyopewa baraka na
Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Sofia Mgema na kuandaliwa na Kigg’s
Entertainment yanatoa nafasi kwa Irene, Jasmeen na Ashura wakipata
tiketi ya kuiwakilisha wilaya hiyo katika mashindano ya Miss Tanga 2009
baadaye Juni.
 
Hii ni mara ya pili kwa wilaya ya Lushoto
kutoa warembo kwa mashindano ya mkoa. Mashindano hayo yalidhaminiwa na
Mercury Finance, Muller Lodge, Studium Restaurant, Kigo Shop, Boznia,
Mahanyu Investiment, Sns Computer Training Center.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents