Habari

Miss Progress atembelea albino Shinyanga

Miss Progress atembelea albino Shinyanga

Mshindi wa Dunia taji la Miss Progress International Julieth William, juzi alitembelea walemavu wa ngozi mkoani Shinyanga. Julieth alitembelea watu hao na watoto wenye ulemavu huo wa ngozi kwa lengo la kutaka kufahamu mahitaji yao kabla ya kuwasaidia.

Ziara hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya One Touch Solutions inayoandaa shindano la Miss Progress Tanzania, na kudhaminiwa na Kampuni ya ndege ya Precision Air na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.

Miss Progress atembelea albino Shinyanga

Mlimbwende huyo aliyetwaa taji hilo mwaka jana nchini Italia alianza kwa kutembelea Shule ya Buhangija, ambayo inatunza maalbino. Akiwa katika shule hiyo alipata fursa ya kutazama mazingira ya shule pamoja na kuzungumza na watoto hao kwa muda wa dakika 30.

Kati ya mahitaji ya watoto hao ni kumaliziwa kwa moja ya bweni lao ambalo bado halijamalizika, ili kuweza kupata nafasi nzuri ya kulala kutokana na lile wanalotumia kuwa dogo. Jambo linalowafanya wabanane kiasi cha wao kulala kitanda kimoja watu watatu.

Baadaye alitembelea ofisi za mkoa za Chama cha Maalbino (TAS) na kuzungumza na watu wazima ili kupata nafasi ya kuyasikia mahitaji yao.

Katika kikao hicho watu hao wenye ulemavu walitaja mahitaji yao yakiwa ni pamoja na kuhitaji kupewa elimu ya ujasiriamali ili waweze kuendesha maisha yao na kuondokana na utegemezi.

Pia alikutana na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga, Eva Lopa, Ofisa Ustawi wa Jamii, Jesca Kagunila.

Baadaye Julieth atakuwa mkoani Mwanza kabla ya kuelekea Arusha.

miss_progress2010

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents