Habari

Miss Rwanda 2019 azua gumzo mitandaoni, Waliowengi wasema hakustahili (+video)

Mshindi wa shindano la Miss Rwanda 2019, Nimwiza Meghan amezua gumzo nchini humo baada ya watu mitandaoni kutoridhishwa na maamuzi ya majaji wa shindano hilo.

Nimwiza Meghan

Nimwiza Meghan

Kabla ya shindano hilo, kufanyika wikiendi iliyopita, mlimbwende
Josianne Mwiseneza ndiye aliyekuwa akipigiwa upatu na watu mitandaoni kwani ngozi yake na ushujaa wa kutoka kijijini hadi mjini kuwania taji hilo.

Josianne Mwiseneza aliteuliwa kuwa Miss Popularity

Josianne Mwiseneza

Josianne licha ya kuwa na muonekano wa kawaida, aliwavutia Wanyarwanda waliowengi kwenye usahili wa shindano hilo, ambapo siku ya tukio hilo alikuwa na jeraha kubwa mguuni na baada ya kuulizwa alijibu kuwa ameumia wakati akijiandaa kuja kwenye usahili huo.

Wanyarwanda wengi walianza kumpa sapoti kwenye mitandao ya kijamii wakiwemo watu wasanii wa muziki kwa kumuita mzalendo.

Alipojieleza ni kitu gani atakifanya kwa Wanyarwanda endapo atatwaa taji hilo, Josianne Mwiseneza alisema kuwa atahakikisha anatokomeza tatizo la utapiamlo kwenye jamii yake.

Mrembo Josianne Mwiseneza sio tu aliwavutia watu mitandaoni bali hata kwa upande wa kura aliongoza kwa kuwaacha wenzake mbali mno, jambo ambalo hakuna ubishi kuwa Wanyarwanda wengi wakiwemo Waandishi wa Habari na Wasanii waliamini kuwa ndiye atakayechukua taji hilo.

Lakini mwisho wa siku mshindi akaja kutangazwa mwingine, nje ya matarajio ya watu wengi.

Josianne alitangazwa kuwa Miss Populality kwenye mashindano hayo, kitu ambacho kilipokelewa kwa shangwe kwenye tukio hilo la utoaji wa taji la Miss Rwanda.

https://youtu.be/lJWQIbHt6DI

Licha ya watu wengi kumsapoti, wapo pia wengine waliomdhihaki dada huyo kwa kumfananisha na wanyama jambo ambalo lilizua chuki baina ya Wanyarwanda.

This image has an empty alt attribute; its file name is DxyZXQDWwAAqRr8.jpg

Kwa mujibu wa ripota wa BBC nchini Rwanda, Yves Bucyana amesema kuwa umaarufu wa Joanne ulichochewa na masuala ya kikabila baina ya Wahutu na Watutsi.

Tayari mamlaka husika za kiserikali nchini Rwanda zimeonya vikali, watu wanaoeneza masuala ya kikabila kupitia kivuli cha Miss Rwanda 2019.

Watu wengi nchini Rwanda kupitia mitandao ya kijamii, wamesema kuwa Josianne alistahili taji hilo kwani uzuri pekee sio kigezo cha kuwa Miss Rwanda na nchini humo hakuna mwanamke mbaya.

Wengine walionekana kuponda mashindano hayo kwa kitendo cha kuchagua wasichana weupe kila mwaka ile hali hawajawahi kutwaa taji lolote la kimataifa.

Kufuatia malalamiko hayo, Majaji wa shindano hilo wamesema “Ni mambo matatu muhimu tunayozingatia, kwanza ni mwenendo wao, jinsi wanaovyotembea ama kujionyesha hapa mbele ya jopo la majaji kwa kifupi maumbile na urembo wao kwa ujumla.Tunaangalia pia jinsi wanavyojieleza kwa maswali tunayowauliza, kuna wanaojiamini kwa kujibu, kuna wanaopaparika na wengine ambao wanatoa majibu yenye maudhui kamili. Hayo yote tunayazingatia kumchagua dada mrembo kuliko wote”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents