Promotion

Miss Tanzania 2007 kupata gari la Sh45m

Vodacom Miss TanzaniaMREMBO atakayetwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2007 atajishindia gari aina ya Toyota RAV 4 lenye thamani ya shilingi milioni 45. Mchuano huo utakaoshirikisha warembo 26, umepangwa kufanyika Septemba Mosi jijini Dar es salaam.

Vodacom Miss Tanzania

 

Na Clara Alphonce

 

MREMBO atakayetwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2007 atajishindia gari aina ya Toyota RAV 4 lenye thamani ya shilingi milioni 45.

 

Mchuano huo utakaoshirikisha warembo 26, umepangwa kufanyika Septemba Mosi jijini Dar es salaam.

 

Meneja wasiliano wa Vodacom, Jacqueline Namfua alisema zawadi hiyo ya gari imetolewa kwa pamoja kati ya Vodacom na Shivacom Tanzania.

 

Mbali na gari hilo, mshindi pia atazawadiwa shilingi milioni 8 na tiketi ya kushiriki shindano la urembo la dunia litakalofanyika Warsaw, Poland. Gari hilo lilionyeshwa kwa warembo na waandishi wa habari kwenye ofisi za Toyota, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.

 

Mbali na zawadi ya mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata sh5,500,000, wa tatu, sh3,500,000 wanne na tano ni sh 2,500,000 na sh 2,000,000. Pia watakaoshika nafasi ya sita hadi 10, Vodacom itawapa sh 1,200,000 kila mmoja na sh 600,000 kwa nafasi ya 11 hadi 26.

 

”Kama tulivyowatangazia hivi karibuni kuwa mwaka huu Vodacom Tanzania imeamua kuongeza zawadi za mshindi wa Vodacom Miss Tanzania kutokana na kuwepo na ushindani na mashindano kupata sura,” alisema Jacquline.

 

Jacquline alisema kuongeza msisimko wa mashindano ya Vodacom Miss Tanzania mshindi pia ana nafasi ya kushinda nafasi ya Vodacom Miss Popularity.

 

“Hii haibagua, hata mshindi wa kwanza anaweza kupata tuzo ya Miss Popularity ambayo mshindi atazawadiwa shlingi milioni 5.”

 

Wakati huo huo, Vicky Kimaro anaripoti, mrembo wa taji la Balozi wa Redd’s ambalo hutolewa na TBL kama wadhamini washiriki wa Miss Tanzania atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 2.5

 

Akizungumza kwenye kambi ya warembo hao iliyopo Beach Comber nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana, Balozi wa Redd’s anayemaliza muda wake Jokate Mwegelo alisema mbali na kiasi hicho cha fedha pia atapata posho ya shilingi 200,000 kila mwezi kwa muda wa mwaka mmoja.

 

Mshindi wa tuzo ya balozi wa Redd’s atatangazwa siku ya fainali ya Vodacom Miss Tanzania.

 

Katika hatua nyingine, washiriki 26 wa kinyang’anyiro cha Miss Tanzania wanatarajia kufanya ziara mkoani Arusha kuanzia Agosti 19 na Agosti 24 watapanda jukwaani kwenye onyesho la mitindo la Redd’s litakalofanyika kwenye Hoteli ya Impala mjini humo.

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents