Habari

Miss Tanzania 2010 Kujulikana

 

Wahu kutoka Kenya anatarajia kupamba katika shindano la kumtafuta mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010, litakayofanyika Septemba 11 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashimu Lundenga alisema kwamba Wahu atasindikizwa na wasanii wa hapa hapa nyumabani  akiwemo AY Ambwene Isaya, Temba ,Chege  pamoja na wasanii kutoka  THT, sambamba kabisa na bendi ya TANZANITE  itakayotumbuiza wageni waalikwa.

Shindano hilo  litawahusisha warembo 30 kutoka  kona zote za Tanzania, ambamo mmoja kati yao atamridhi Miriam Gerald,Miss Tanzania 2009. KAMATI ya Miss Tanzania imewatangaza majaji tisa watakaousika katika uteuzi wa kumchagua mrithi wa Miriam Gerarld Miss Tanzania 2010 katika shindano litakalofanyika Septemba 11, katika ukumbi wa Mlimani City.

Lundenga aliyataja majina ya majaji yaliyopendekezwa na Basata  ni Richard Magongo kutoka TBL; Benard Mrunya kutoka Ngorongoro Crater; Devota Mdachi, TTB;  Ayobu Rioba,   Misa;  Michale Shilla , Basila Mwanukuzi, Miss Tanzania 1998; John Njoroge kutoka Corridor Spring Hotel Arusha, Stella Kiwango, Vodacom na Prashant Patel Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania.

Mshindi katika shindalo hilo ataondoka na gari haina ya Hyundai  i10 na milioni 10, huku mshindi wa wa pili 6.2 milioni, wa tatu na wanne ataondoka na 2.4m na wa tano mpaka wa 10 watapata milioni 1.4 waliobaki wa 11-30 watapata laki 700,00 kilammoja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents