Burudani

Miss Tanzania Aagwa

Mwakilishi  wa Tanzania katika mashindano ya Miss World Genevive Mpangala,amekabidhiwa bendera na Mama Esther Mkwizu ambaye ni Mwenyekiti wa Sekta Binafsi , aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Akimkabidhi bendera hiyo Mama Mkwizu alimtaka mrembo huyo wa Tanzania kujiamini na kuiletea heshima Tanzania kwa kuwa mwenye nidhamu ya hali ya juu na kujituma ili kuweza kufika mbali zaidi ya warembo wa Tanzania waliomtangulia.

Katika hafla hiyo ambayo iliyofanyika katika ofisi za kituo cha uwekezaji  ilihudhuriwa na afisa habari masoko wa wadhamini wakuu wa shindano la Miss Tanzania Vodacom,  Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji TIC bwana Emanuel Ole Naiko, Mkurugenzi wa utamaduni na kaimu katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni na michezo Prof  Helmans Mwansoko pamoja na wazazi wa mrembo huyo Bwana na Bibi Mpangala.

Genevieve anatarajiwa kuondoka kesho mchana na ndege ya shirika la Qatar airways kuelekea jijini Sanya nchini China ambako shindano la dunia Miss World 2010 linatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents