Bongo MovieBurudani

Miss Tanzania Diana Edward kufuata nyayo za Wema Sepetu

Miss Tanzania 2016/7 Diana Edward ameweka wazi yupo mbioni kuingia katika tasnia ya uigizaji wa filamu nchini [Bongo Movie] kama alivyofanya aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu.

Diana Edward

Mrembo huyo amesema lengo la kuingia katika uigizaji, nikutaka kubadilisha mtazamo wa Watanzania kuwa nchini hakupatikani filamu zenye ubora au hazipo habisa, na yeye atajikita katika uigiaji wa filamu za action.

Wema Sepetu

“Kila kitu kipo tayari, nimeshafanya mazoezi sasa hivi nasubiria mambo yangu yakikaa sawa nianze kutengeneza. Napenda action movie kwa sababu am so addicted in action movie, staki kusema mengi sana kwa sababu nasubiria maamuzi kutoka kwa meneja wangu itakuwaje, kwa hiyo msubiri,” amekiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Mimi nilikuwa naigiza kuanzia muda mrefu ingawa sikutoa movie yoyote,” ameongeza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents