Miss Tanzania Kutoa msaada kwa Yatima Arusha
Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, anatarajia kutoa msaada kwa watoto yatima katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kama zawadi ya sikukuu ya Krisimas.
Genevieve ambaye anatarijia kuondoka jijini Desemaba 15, kuenda Arusha kwa shughuli hizo amesema tayari maandalizi yamekwisha malizika.
Aliongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa anatarajia kuondoka na warembo 12 ambao walishiriki mashindano ya urembo mwaka huu ambao ni Glory Mwanga , Christine Justine, Consolata Lukosi, Bururi Ibrahimu, Wande Magese Salma Mwakalukwa., wengine ni Anna Daudi, Asimu Malik, Furaha Davidd, Pendo Sam, Prisca Mkoyi pamona na Fatuma Ibrahimu.
Genevieve aliongeza kwa kusema kuwa Mrembo wa mwaka 1997 Saida Kessy ndiye aliyefanya kazi ya kutafuta vituo vya watoto yatima na kusema hii ni moja kati ya mikakati yake ya kufanya kazi za jamii katika kuwasaidia na kutoa msaada.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya LINO Hashimu Lundenga alisema jumla ya milioni kumi itatumika katika zoezi hilo ikiwa ni lengo la kutimiza mipango ya urembo wenye malengo maalum.