Habari

Miss Ukonga 2009

Miss Ukonga 2009
Kwa mara nyingine tena Bongo5 Media Group(T) Ltd. imefanikisha kumpata
mrembo wav Vodacom Miss Tanzania katika ngazi ya kitongoji, shindano
hilo ambalo lilikuwa la kumsaka mrembo wa kitongoji cha ukonga
lilishuhudia  Nshoma Nkwabi akijinyakulia nafasi ya ushindi wa Kwanza
akifuatiwa na Doris Jimmy nafasi ya pili na Zena Rashidi nafasi ya tatu.

Shughuli hiyo ya kumsaka mnyange wa kitongoji cha ukonga ilifanyika usiku wa ijumaa katika ukumbi wa Hill-Tech Resort na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki wa mashindano ya urembo ambao waliridhishwa na mnyange mpya wa kitongoji hicho.

Aidha shughuli hiyo ya kumsaka mrembo wa kitongoji cha Ukonga ilipambwa na burudani kutoka bendi ya Diamond Musika ila kama kawaida ya BONGO5 katika kuwapa wadau burudani mahiri Chidi benz alifanya suprise la nguvu na kuunyanyua ukumbi mzima.

Shindano hilo liliandaliwa na Bongo5 Media Group (T) Ltd chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania, Redds Premium cold na Clouds Fm lilihudhuriwa pia na miss Tanzania wa mwaka 2006 Nancy Sumari na mwigizaji wa filamu Cheni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents