Habari

Miss Universe yaishia Hivi

Miss Universe 2007Ni mrembo kutoka Japan, Riyo Mori (20) ndie ayetawazwa kuwa Miss Universe 2007 na kuwanwaga warembo wengine kutoka nchi tofauti duniani walioshiriki kinyang’anyiro hicho

Miss Universe 2007Ni mrembo kutoka Japan, Riyo Mori (20) ndie ayetawazwa kuwa Miss Universe 2007 na kuwanwaga warembo wengine kutoka nchi tofauti duniani walioshiriki kinyang’anyiro hicho.


Mrembo kutoka Brazil ndie alyefanikiwa kumfuatia Riyo na Mrembo kutoka Venezuela akishika nafasi ya tatu, huku duru la tano bora likifungwa na Mrembo kutoka Korea aliyeshika na fasi ya nne na Mrembo kutoka USA alishika ya tano.


Nae mrembo wetu Flaviana na Matata aliyeiwakilisha nchi yetu alifanikiwa kuingia 10 bora ambapo aliongozwa na Mrembo kutoka India,Akifuatiwa na Angola kisha yeye (Flaviana) Mrembo kutoka Nikaragua na Mrembo kutoka Mexico ndiye aliyekamilisha 10 bora.


Kwa nafasi hiyo aliyoipata Flaviana kwa nchi kama Tanzania ambayo ni mara ya kwanza kushiriki katika shindano hili, imetupa moyo na tunaichukulia kama ni ushindi kwa namna moja au nyengine.


Mbali na Flaviana kuinga 10 bora vyombo kibao vya habari duniani vimemsifu kuwa ameitangaza Tanzania vizuri saana hasa kwa mtindo wake wa Nywele wa kipara…kwani yaonyesha katika historia ya mashindano hayo ni mrembo pekee aliyeshiriki shindano hilo akiwa na kipara.


Flaviana amerudi nchini jana na amepokelewa na wadau wa shindano hilo.


Flaviana

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents