DStv Inogilee!

Miss World ashiriki kupanda miti nchini Kenya

Miss World 2011 Ivian Sarcos kutoka Venezuela amemaliza ziara yake nchini Kenya kwa kujihusisha na masuala ya kibinadamu yakiwemo upandaji miti.

Ivian Ivian Sarcos aliyezaliwa July 26, 1989 na ambaye ni mwanamke wa kwanza kushinda taji la Miss World kutoka Venezuela tangu Jacqueline Aguilera mwaka 1995, jumamosi iliyopita alimvisha taji mshindi wa Miss World Kenya Shamin Nabil, 20.

Pamoja na kupanda miti, mlimbwende huyo pia aliwatembelea wanawake wajasiriamali wanaojihusisha na kazi za mikono pamoja na vyuo vya ufundi.

Kabla ya kwenda nchini Kenya Ivian alikuwa nchini Ghana ambapo ratiba ya safari yake ilianza May 19 hadi jana May 28.

Mpaka sasa mrembo huyo ameshazitembelea China, Ufaransa ,Ghana, Hong Kong, India, Indonesia, Ireland, Kenya, Urusi, Uingereza, Marekani na kwingineko.

Nchini Kenya Iviana aliambatana na CEO wa Miss World Ltd Julia Morley, Miss World Caribbean, Amanda Vilanova na Miss World Europe, Alize Lily Mounter.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW