Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Misuli yamuangusha Usain Bolt uwanjani (+Video)

Mwanariadha maarufu duniani, Usain Bolt jana aliumia na kushindwa kumaliza mbio zake za mwisho za ubingwa wa dunia jijini London baada ya kubanwa na misuli akiwa uwanjani.

Usain Bolt akiwa ameanguka baada ya kubanwa na misuli.

Bingwa huyo wa medali 11 za dhahabu alibanwa na misuli na kulazimika kuondoka uwanjani alipokuwa akikimbia mbio za kupokezana vijiti za 4x100m ambazo timu ya Uingereza iliibuka kidedea.

Akiwa uwanjani Bolt alionekana kuchechemea hadi kuanguka chini kunako sekunde za mwisho za mbio hizo za kupokezana vijiti.

Hata hivyo daktari wa timu ya taifa ya Jamaika,  Kevin Jones amesema sababu za Mwanariadha huyo kubanwa na misuli ni hali ya hewa ya London pamoja na ubovu wa ratiba wa mbio hizo ambapo wachezaji walifika mapema lakini walikaa lisaa limoja nje ya ratiba ilivyopangwa kitu ambacho kiliwaathiri wakimbiaji wake.

Bolt alikuwa na matumaini kwamba angestaafu maisha yake ya ukimbiaji kwa kushinda medali mbili kwenye mashindano hayo ya kimataifa lakini ameondoka na medali moja ya shaba pekee aliyoshinda kwenye mbio za mita 100 wiki iliyopita.

https://youtu.be/vAQLqYKTFsU

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW