Burudani

Mitaa Inasema: Bifu la Sugu na Ruge lawaka upya


Bifu ambalo lilimalizika hivi karibuni kati Ruge Mutahaba na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu linasadikiwa kurudi upya baada ya kukosekana kwa maelewano, pamoja na kitendo cha mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group kuwashitaki wasanii wawili wa Anti Virus James Kasulwa na Levinson Kasulwa maarufu kwa jina la Mapacha.

Baadhi ya wasanii ambao wamelizungumzia bifu hilo ni Mkoloni na kusema, yeye hakuhusika kwenye makubaliano yaliyofanyika kati ya Ruge na Sugu. Amesema lakini alipokwenda kuangalia makubaliano hayo, aligundua hayakuwa na maslahi kwao na kuamua kusimama upande ule ule. Msanii mwingine G Solo naye alisema kwamba hadi sasa yeye hajui kwanini wasanii wenzake wawili ‘Mapacha’ walishitakiwa, hivyo kwake anaona maelewano hamna, na bado ataendelea vita kama kawaida.

Wakati huo huo Sugu naye alipoulizwa kuhusu makubaliano hayo, alisema kwamba kwa sasa yupo kwenye uchaguzi mdogo Arumeru, kwa hiyo akishamaliza na atakaporudi ataongelea kwa kina mambo hayo. Hali hii imepelekea kuhisi kwamba mgogoro huo umerudi tena. Wasanii hao ‘Mapacha’ watafikishwa katika mahakama ya Kisutu leo, saa saba mchana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents