Habari

Mitandao ya Facebook, LinkedIn yaongoza kwa kuvunja ndoa za watu

Mitandao ya kijamii ya Facebook na LinkedIn inaongoza kwa kuvunja ndoa za watu duniani kwa wanandoa kuwa na mahusiano na watu zaidi ya mmoja mitandaoni.

Hayo yamesemwa na Mwanasheria Abigail Lowther, kutoka katika kituo cha Wanasheria cha Hall Brown Law Family cha nchini Uingereza.

Bi. Lowther amesema kwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 kesi za madai ya taraka zimeongezeka kutoka kesi 40 hadi 50 kwa mwaka 2015 hadi kufikia kesi 65-85 kwa mwaka 2017. Chanzo chake ni mitandao ya kijamii, ambapo facebook na LinkedIn imeongozwa kutajwa kwenye kesi hizo.

Mwanasheria Lowther amesema  wateja wake wengi wanaokuja kwenye kituo hicho wanalalamikia kukua kwa teknolojia kunavyoathiri mahusiano yao na kukosekana kwa amani kwenye ndoa.

Unajua Teknolojia inawafanya watu wawe karibu kwa njia ya kutumiana meseji, picha na hata video hii inafanya hata wanandoa kusalitiana wakiwa kwenye kitanda kimoja , Ingawaje kuna baadhi ya wanawake hukiri wazi kuwa wanapokuwa mitandaoni hupatwa na vishawishi vingi ikiwemo jumbe za mahaba na picha za kikubwa kutoka kwa wanaume mbalimbali hivyo husababisha waume zao kuondoa imani kwao,“amesema Bi. Lowther kwenye mahojiano yake na gazeti la The Telegraph.

Joan Pratt ni moja ya Waasisi wa kituo hicho na ni Mwanasheria wa masuala ya ndoa aliambia gazeti la The Telegraph kuwa “Wapenzi wengi huchepuka kwa kukusudia mitandaoni ila wanajisahau kufuta meseji na picha wanazotumiwa na watu wao ni jambo geni kwenye ulimwengu wa teknolojia lakini hatuna budi kuangalia namna ya kulitatua kabla ya kuwa tatizo kubwa.

Vyanzo vingine vimetajwa kuwa tovuti na App za ngono zimechangia watu kuchepuka kwenye ndoa kwa kiasi kikubwa nchini Uingereza.

Tafiti zinaonesha kati ya ndoa 1,166 nchini Uingereza kwa mwaka ndoa 987 zinasuluhisha matatizo yanayotokana na mitandao ya kijamii huku ndoa 60 hadi 70 zikivunjika kabisa.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents