Habari

Miti Milioni 280 kupandwa na Serikali kila mwaka

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira imelenga kupanda miti zaidi ya milioni 280 kila mwaka katika maeneo yaliyo katika hatari za kukabiliwa na hali ya jangwa na ukame.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na Ukame Duniani inayofanyika tar 17 Juni kila mwaka.

“Ukataji wa miti kiholela na uharibifu wa misitu unaosababishwa na utegemezi mkubwa wa binadamu wa kupata mahitaji kutokana na mazao ya misitu pamoja na huduma zingine muhimu,kunazidisha ukubwa wa tatizo hili,” alisema Makamba

Aidha alisema ili kupunguza utegemezi katika Maliasili Kwa mfano programu ya kitaifa ya upandaji miti ya mwaka 2016 hadi 2021 inalenga kupanda miti zaidi ya milioni 280 kila mwaka na inalenga hasa maeneo yaliyo katika hatari za kukabiliwa na hali ya jangwa na ukame.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ardhi ni Makazi yetu Tuitunze kwa manufaa ya baadaye hivyo wananchi wote washiriki kikamilifu katika kuitekeleza ili kuhakikisha ardhi yetu inatunzwa kwa ajili ya kizazi kijacho.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents