Burudani

Miwani ya Paul Walker iliyopatikana eneo la ajali kupigwa mnada

Baadhi ya vitu vinavyodaiwa vilichukuliwa kutoka katika eneo la ajali ya gari iliyosababisha kifo cha star wa filamu ya ‘Fast & Furious’ Paul Walker mwishoni mwa mwaka jana, vinatarajiwa kupigwa mnada.

Paul walker-3

Vitu hivyo ni pamoja na miwani ya jua inayodaiwa alikuwa ameivaa siku hiyo kabla ya ajali, chombo cha kuzimia moto (fire extinguisher) kilichotumika kujaribu kuuzima moto baada ya ajali.

Kwa mujibu wa New York Daily, mtaalam wa kampuni ya minada BidAMI.com amesema mtu aliyewapelekea vifaa hivyo alidai kuwa aliviokota vichakani karibu na eneo ilipotokea ajali, na alipojaribu kuwasiliana na familia ya Walker hawakuonesha nia ya kuvichukua.”We photo-matched them to the one’s Paul was wearing [that day].”

Sehemu ya fedha zitakazotokana na mnada wa vifaa hivyo zitapelekwa savethemustangs.org kwaajili ya charity.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents