Habari

Mji wa kale wagundulika Ethiopia

Wataalamu wa mambo ya kale wamegundua mji wa kale ambao ulikuwa umesahaulika mashariki mwa Ethiopia.

Wakulima katika eneo hilo la Harlaa wamekuwa wakipata vitu vya ajabu, kama vile sarafu kutoka China kwenye mashaba yao, kitu kinachovuta hisia za watu kuwa huwenda palikuwa makazi ya watu wa zamani (Majitu).

Katika karne ya 10 inadaiwa kuwa mji pia ulikuwa ni kitovu cha biashara, kumegundulika sarafu za fedha na shaba  zilizotumika  karne ya 13  katika nchi ya Misri, pamoja na vito kutoka Madagascar, Maldives, Yemen na China.

Miongoni mwa vitu vilivyogunduliwa eneo hilo ni pamoja na msikiti ambao inakadiriwa ulijengwa karne ya 12, pamoja na makaburi ambayo yalitumiwa na Waislamu waliokuwa wanaishi eneo hilo.

Mkuu wa utafiti huo ameeleza kuwa wamekuta muundo wa msikiti eneo hilo ambao unashabihiana na ule uliogundulika kusini mwa Tanzania.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents