Habari

Mji wa Norway ambao haujawahi kupata jua la masika kwa miaka 100 unatarajia kupata jua la ‘kutengenezwa’ hivi karibuni

Wakazi wa mji wa Rjukan nchini Norway ni kati ya watu ambao wanategemea kupata jua la masika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha masika, baada ya mji huo kutopata jua la moja kwa moja kwa miaka 100 sasa katika kipindi hicho.

jua la kioo

Ili kuondokana na giza na baridi katika kipindi cha msimu wa ‘winter’ halmashauri ya mji huo imetumia zaidi ya pesa ya Norway kronor milioni 5 (zaidi ya billioni 1) kuweka vioo tatu vikubwa ‘heliostats’ vilivyotegeshwa juu ya bonde ikiwa ni mita 450 juu ya mji vitakavyomulika jua halisi na kumulika katika mji huo.

jua la kioo-2

Helikopta zitatumika kufunga vioo hivyo na zitakuwa zikifuatilia mwenendo wa jua na kumulika mwanga moja kwa moja katika ‘main square’ ya mji wa Rjukan ili kuwasaidia wakazi wa mji huo mdogo ambao wamekuwa wakifunga safari kila mwaka kwenda juu ya mlima mrefu ili kupata joto la jua halisi.

Tazama jinsi helikopta zitakavyokuwa zikifanya zoezi hilo la kuzungusha vioo vya kumulika jua katika mji huo

SOURCE: DAILY MAIL

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents