Mjumbe aomba kuombewa ulinzi wa Mungu

MBUNGE wa Nzega (CCM), Lucas Selelii, amesema wajumbe wa kamati wamejitoa mhanga na kuwaomba wabunge kuwaombea kwa sababu vitisho wanavyopata ni vikali.

Na Midraji Ibrahim, Dodoma

 

 

 

MBUNGE wa Nzega (CCM), Lucas Selelii, amesema wajumbe wa kamati wamejitoa mhanga na kuwaomba wabunge kuwaombea kwa sababu vitisho wanavyopata ni vikali.

 

 

 

Selelii alisema, maisha yao yako hatarini na wana ushahidi ambao

 

watamkabidhi Spika wa Bunge, Samwel Sitta ili wakapadhurika warejee kwenye kumbukumbu.

 

 

 

Alisema kamati hiyo ilimtanguliza Mungu na kuamua kutumia uzalendo na ujasiri kwa sababu, walikuwa wakipata vitisho vingi.

 

 

 

Alipendekeza bunge kutoa onyo kali kwa wale waliokuwa wakipanga watumishi wa serikali kwenye kamati kusema uongo.

 

 

 

Selelii ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura uliypipa ushindi Kampuni ya Richmond Development, alipendekeza kuwa Bunge litoe onyo kali kwa viongozi waliokuwa wanafundisha kwenda kusema uongo mbele ya kamati.

 

 

 

�Bunge lako litoe onyo kali sana kwa wale waliokuwa wakipanga watumishi wa serikali kuja kusema uongo mbele ya kamati kwani tulikuwa tunamwona mtu ana unyonge ndani ya moyo wake…,� alisema.

 

 

 

Onyo lingine alipendekeza wapewe watumishi wa serikali waliodiriki kuinyima kamati yao majalada.

 

 

 

Kuhusu Takukuru, Selelii alisema taarifa waliyotoa ni sawa na barua iliyoandikwa usiku kwa ajili ya kuwahi vyombo vya habari, hivyo akapendekeza kuwa Mkurugenzi wa Takukuru na maafisa wanne wa taasisi hiyo walioshiriki kwenye uchunguzi huo wawajibishwe mara moja.

 

 

 

Pia aliitaka serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa kwenye kikao kijacho kuhusu usajili wa Richmond na kwamba jalada walilopewa ni la kughushi.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents