Michezo

Mkali wa NBA atua Dar

Mchezaji wa zamani wa wa timu ya taifa ya Marekani Steve Smith anatarajiwa kuwasili leo nchini kwa ajili ya kuendesha ‘Sprite Basketball clinic’.

Smith ambaye pia aliwahi kuchezea timu za Atlanta Hawks na Miami Heat, zote za ligi maarufu ya mchezo wa kikapu Duniani (NBA) ana historia ya kucheza na mchezaji nyota Michael Jordan.

Akizungumza jijini Dar, makamu mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) Phares Magesse, amesema lengo kubwa la kumleta mchezaji huyo nchini ni kuuendeleza na kuukuza mchezo huo wa mpira wa vikapu kwa vijana nchini.

Smith ataendesha mafunzo hayo kwa muda wa siku mbili ambazo ni ijumaa na jumamosi katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es Salaam. Wakati huo huo Magese amesema mafunzo ya siku 10 ya ukocha yalioandaliwa na TBF kwa kushirikiana na shirikisho la kikapu la kimataifa (FIBA) yameanza jana katika viwanja vya Bon Bosco vilivyopo upanga jijini Dar.

Alisema mafunzo hayo yanaendeshwa na mkufunzi anayetambuliwa na FIBA Samuel Wanjohi kutoka Kenya ambapo lengo kubwa ni kuwapa elimu makocha hao.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents