Mkali Wenu amchambua Alikiba, adai Mvumo wa Radi si sawa na Seduce Me (+Video)

Mchekeshaji Mkali Wenu amezungumzia ujio wa Alikiba ulioambatana na ngoma yake mpya ‘Mvumo wa Radi’.

Mkali Wenu na Monalisa

Mkali Wenu amesema ngoma ‘Mvumo wa Radi’ Alikiba alivyoitoa ni tofauti na ilivyokuwa Seduce Me.

“Ukweli ni kwamba kuna tofauti alipotoa wimbo wa Seduce Me na hii mpya, wakati wa Seduce Me kulikuwa na vitu vingi, mara Diamond kasema vipusa vitu hivvyo vilikuwa vingi kwa hiyo watu wakawa attantion kusubiria Alikiba atafanya kitu gani,” Mkali Wenu ameiambia Bongo5.

“Baada ya kutoa watu wakaona kidume kafanya kitu lakini sasa hivi katoa hakuna skendo yeyote, Mange hajaposti kama ilivyokuwa Seduce Me, imeenda lakini si kama ilivyokuwa mzuka wa mwanzo,” amesisitiza.

Ni kweli ngoma ya Alikiba Mvumo wa Radi ni tofauti na Seduce Me kwani ngoma hii ilikuwa nchini ya Sony Music International ndio sababu ikawekwa Vevo na sio YouTube kama ilivyo Mvumo wa Radi ambayo imetoka kwa ajili ya kutambulisha kinywaji chake cha Mo Fanya.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW